SlideShare une entreprise Scribd logo
1  sur  9
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 1
MKATABA WA AJIRA
MKATABA HUU unafanyika leo tarehe ………… mwezi …………………., 2014.
BAINA YA
… … … … … … … … … … …, wa S.L.P ………………… (ambaye katika Mkataba huu
atajulikana kama “Mwajiri”) wa upande mmoja wapo wa Mkataba
NA
… … … … … … … … … … … , wa S.L.P ………………….. (ambaye katika Mkataba huu
atajulikana kama “Mwajiriwa”)
Namba ya Ajira (I.D).
Umri: Jinsia:
NSSF Na: Dini:
Tarehe ya kuzaliwa: Sehemu ulipozaliwa:
Jina la Mke: Tarehe aliyozaliwa Mke:
Jina la Mtoto/Watoto: Tarehe ya kuzaliwa Mtoto/Watoto:
1.
2.
3.
Dealing with:-Radio Broadcasting, P.A. system and General
Entertainment
P.O. Box 70270 DAR ES SALAAM TEL: +255 26 2701114 Fax +255 26 2701115,
Mob: +255 784 877788, Email: radioebony@ebonyfm.com
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 2
MTU WA KARIBU; Jina kamili: … … … … … … … … … … … … … … Umri … … … …
Anuani/Mawasiliano: S.L.P … … … … … Simu … … … … … … … …
Anapoishi sasa: … … … … … … … Makazi ya kudumu … … … … … .
AMBAPO
1. Mwanzo
(a) Mwajiri ni Kampuni iliyopo Iringa inayoshughulika na Matangazo ya Radio.
(b) Mwajiriwa anafanya Shughuli Iringa na sehemu yeyote atakayopangiwa na mwajiri wake ndani
ya utaratibu wa kazi.
2. Wakati wa kuanza kazi
2.1 Mwajiri anakusudia kumwajiri kwa muda wa mwaka/miaka … … … … … mwajiriwa, endapo
mkataba huu utaisha utaongezwa/utaendelea kwa matakwa ya kampuni.
2.2 Mahali ulipoajiriwa … … … … … … … … … … …
2.3 Kituo cha kazi … … … … … … … … … … … … ..
2.4 Kazi zako
2.4.1 Nafasi kazini … … … … … … … … … … …
2.4.2 Ripoti kwa … … … … … … … … … … … …
2.4.3 Kazi utapangiwa na … … … … … … … … …
Mwajiriwa anakubali matakwa ya mwajiri na anakubali kwa hiari yake mwenyewe kuajiriwa kwa
muda wa mwaka/miaka … … … … … kama … … … … … … … … … …
3. Majaribio
3.1 Mkataba huu wa ajira unatambua mda wa majaribio usiopungua miezi mitatu (3) toka siku
mwajiriwa alipopata ajira husika. Lengo la mda wa majaribio ni kumpima mwajiriwa kama
anakidhi vigezo na viwango vya nafasi/kazi husika. Kama mkataba huu utavunjwa ndani ya
mda wa majaribio mwajiriwa atapewa notisi ya maandishi ya siku saba ya kuvunjwa kwa
mkataba huu.
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 3
3.2 Mda wa majaribio unaweza kuongezwa au kupunguzwa na mwajiri pale atakapoona ni vyema
kufanya ivyo, Mwajiri anaweza kuongeza mda wa majaribio hadi miezi kumi na miwili (12).
3.3 Kikomo cha mda wa majaribio, Mwajiri atatakiwa kumfahamisha mwajiriwa kwa maandishi
kuchaguliwa kwake katika ajira, kama tu akupata taarifa katika mkataba wake, mwezi mmoja
baada ya kuisha mda wa majaribio.
4. Ujira
4.1 Kima cha malipo ya jumla kabla ya makato ya kisheria ni Tshs ….…………. kwa mwezi
kulingana na masaa 45 ya ufanyajikazi kwa wiki au kwa taswira ya kampuni husika.
4.2 Mwajiriwa atakatwa makato yanayotambulika kisheria;
- Mifuko ya Jamii (NSSF) au Mfuko wa chaguo lako.
- Pay As Your Earn (P.A.Y.E).
- Sahihi ... ... ... ... ... ... ... ... ...
4.3 Mwajiriwa atatakiwa kuwa na akaunti ya benki, kwajili ya malipo ya Ujira wake;
4.4 Akaunti ya Benki … … … … … … … … … … … … … … … … … ...
5. Saa za kazi
5.1 Mda wa kazi kwa ujumla ni masaa 45 kwa wiki, ila kutokana na taswira na muundo wa
kampuni, haswa kituo cha matangazo mwajiriwa atatakiwa kufata Taratibu na Kanuni
zilizowekwa na kampuni husika bila kudhuru kifungu chochote cha mkataba huu.
5.2 Mwajiriwa atatakiwa kutambua kituo hichi cha Matangazo kinafanya kazi masaa ishirini na nne
(24) kwa siku saba(7) za wiki, ivyo sikukuu za umma zikiangukia katika siku za kazi
hakutokuwa na malipo ya ziada au mapumziko kwa watangazaji wa vipindi husika katika siku
hiyo.
5.3 Kila mwajiriwa atapata siku moja (1) ya mapumziko ndani ya wiki (siku saba) kulingana na
atakavyopangiwa na mkuu wake wa Idara.
6. Likizo
6.1 Mwajiriwa ana haki ya kupata likizo ya siku zisizopungua 28 katika mzunguko wa likizo ya kila
mwaka, siku hizo zitajumuisha sikukuu za umma zitakazoangukia ndani ya likizo husika. Likizo
itatolewa ndani ya miezi kumi na miwili (12) toka kuanza kwa ajira yako. Au baada ya kuisha
kwa mzunguko wa awali katika ajira.
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 4
6.2 Likizo itatolewa na mwajiri pale atakapoona ni wakati mwafaka kufanya ivyo, na kumjulisha
mwajiriwa.
6.3 Idadi ya siku za likizo zinaweza kugawanywa na mwajiri katika mda tofauti ndani ya mzunguko
wa likizo bila kudhuru idadi ya siku za likizo za mfanyakazi.
6.4 Mwajiri hatoomba au kuombwa na mwajiriwa kufanya kazi ndani ya mda wa likizo.
7. Likizo ya Ugonjwa
7.1 Kulingana na kifungu cha 32 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (Sheria kuu) Sura ya
366, mwajiriwa atapata likizo ya Ugonjwa kwa siku 126 katika mzunguko wa likizo na malipo
yake halali, ikiwa tu, ugonjwa huo umethibitishwa na vyeti cha tatibu aliesajili au tabibu
anayekubalika na mwajiri.
7.2 Likizo ya Ugonjwa iliyotajwa katika kifungu kidogo cha (1) italazimika kukokotolewa kama
ifuatavyo;
7.2.1 Siku 63 za kwanza zitatakiwa kulipwa mshahara mzima,
7.2.2 Siku 63 zinazofuata zitatakiwa kulipwa nusu mshahara
7.2.3 Mwajiri ana haki ya kuvunja mkataba wa ajira baada ya siku 126 za likizo ya Ugonjwa
kupita.
7.2.4 Mwajiriwa anatakiwa kutoa taarifa za ugonjwa haraka iwezekanavyo kwa mwajiri.
8. Likizo ya Uzazi
8.1 Mfanyakazi atalazimika kutoa notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo
ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua na notisi hiyo italazimika
kuambatana na cheti cha kitabibu.
8.2 Vile vile Mwajiriwa atatakiwa kufata taratibu zote za Likizo ya Uzazi kama ilivyoanishwa
katika kifungu cha 33 – kifungu kidogo (2) hadi (11), Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini
(Sheria kuu) Sura ya 366.
9. Likizo ya uzazi ya baba na aina nyingine za likizo
9.1 Wakati wa Mzunguko wa likizo, Mfanyakazi atakuwa na haki ya;
9.1.1 Angalau siku 3 za likizo ya uzazi ya baba kama-
(a) Likizo itachukuliwa ndani ya siku saba za kuzaliwa mtoto na;
(b) Mfanyakazi ni baba wa mtoto;
9.1.2 Angalau siku 4 za likizo kwa sababu zifuatazo;
(a) Ugonjwa au kifo cha mtoto wa mfanyakazi;
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 5
(b) Kifo cha mke wa mfanyakazi, wazazi, bibi na babu, mjukuu au kitukuu.
Mwajiri anaweza kuhitaji uthibitisho wa kawaida wa tukio lolote lililotajwa hapo juu.
10. Kusitishwa kwa Ajira
10.1 Mkataba huu unaweza kusitishwa na pande zote mbili kwa notisi ya siku zisizopungua
28.
10.2 Notisi inatakiwa kutolewa kwa maandishi, ikieleza sababu na tarehe ya kusitishwa ajira
husika.
10.3 Endapo mwajiri atasitisha ajira, anatakiwa kumpa mfanyakazi Cheti.
10.4 Hata ivyo, Mwajiri ana haki ya kutotoa Cheti hadi pale Mfanyakazi atakaporudisha mali
au thamani yeyote ya kampuni.
10.5 Mwajiri atasitisha ajira husika endapo mfanyakazi atashindwa kufata matakwa ya
mkataba huu, taratibu, kanuni na miongozo ya kampuni.
11. Malipo ya Kiinua Mgongo
11.1 Mfanyakazi ana haki ya kupata kiinua mgongo cha mshahara angalau wa siku 7 kwa kila
mwaka ulioisha wa utumishi wa moja kwa moja na mwajiri mpaka kwa kiwango cha juu cha
miaka kumi (10),
11.2 Mwajiri atatakiwa kumlipa kiinua mgongo wakati wa kusitisha ajira ikiwa;
(i) Mfanyakazi amemaliza miezi 12 ya utumishi wa moja kwa moja na mwajiri
11.3 Mfanyakazi hatopata kiinua mgongo kama;
11.3.1 Kama ajira yake ilisitishwa kwa utovu wa nidhamu
11.3.2 Kama amegoma kufanya kazi alizopangiwa kwa taratibu za ofisi
12. Biashara Binafsi
12.1 Wafanyakazi wote ni waajiriwa wa kudumu, ivyo mfanyakazi yeyote hatoruhusiwa
kufanya biashara wakati wa kazi au mda wa kazi.
12.2 Kwenye jengo la kampuni;
12.3 Au kutumia mali, au chombo chochote cha kampuni kuwezesha biashara yake;
12.4 Au kuwatumia waajiriwa wengine wa kampuni hii kufanikisha biashara yake ndani ya
mda wa kazi. Hairuhusiwi.
13. Usiri
13.1 Uendeshaji wa biashara, utendaji na mipango ya kampuni ni vitu vinavyohitaji usiri wa
hali ya juu, ivyo nyaraka, taarifa, kumbukumbu za kimaandishi, muktasari wa vikao vya ndani,
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 6
ulipaji wa mishahara, uendeshaji wa kampuni utalindwa kwa usiri mkubwa, na chochote
hakitakiwi kumhusisha mtu hasie wa kampuni bila idhini ya utawala. Ukibainika kuvunja usiri
huu unaweza kupoteza ajira yako.
14. Utoro
14.1 Mfanyakazi hatotakiwa kukosa kazini katika siku za kazi bila ruhusa ya mwajiri au
uongozi husika.
14.2 Mfanyakazi akitoweka/utoro kazini bila taarifa katika siku tano (5) za kazi, mwajiri
atahesabu upotevu/usitishwaji wa ajira ya mfanyakazi huyo toka siku ya kwanza ya utoro huo
14.3 Mimi, … … … … … … … … … … … … … … natambua utoro kazini utapelekea
kupoteza ajira yangu, natambua kutoonekana kazini kwa siku zisizopungua tano(5) ni uvunjifu
wa mkataba na taratibu za ofisi, ivyo kampuni ihesabu utoro wangu ni sehemu ya kujiuzulu.
14.4 Utoro wa vikao vya alhamisi mara tatu (3) ndani ya mwezi moja (1) vilivyowekwa kwa
utaratibu wa kampuni, unaweza kukufikisha katika kamati ya nidhamu au kukusabishia rekodi
hafifu ndani ya mwaka wa ajira, ivyo kuchangia kupoteza ajira yako.
15. Utovu wa Nidhamu
15.1 Wafanyakazi wote wanatakiwa kuheshimu na kufata sheria, taratibu na kanuni za
kampuni. Mwajiriwa yeyote atakae shindwa kuheshimu taratibu hizo atachukuliwa hatua kali za
inidhamu, au kupoteza ajira yake.
16. Masharti ya Ushindani
16.1 Kulingana na taratibu na kanuni na sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, mfanyakazi
yeyote atapaswa kufata taratibu za kusitisha ajira, endapo mfanyakazi halali wa Redio Ebony
FM mwenye mkataba atatoroka na kwenda kufanya kazi sehemu nyingine bila kufata utaratibu
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
16.2 Mfanyakazi yeyote hatoruhusiwa kufanya kazi yenye mfanano na kampuni hii akiwa
ndani ya ajira husika.
16.3 Ni kosa kwa mfanyakazi wa Ebony FM kufanyakazi na kituo kingine cha matangazo
akijua yeye ni mwajiriwa wa halali wa kampuni tajwa.
16.4 Kufanya au kuuza vipindi, vionjo au muundo wa vipindi vya kampuni ni kosa kisheria,
hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakaebainika.
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 7
17. Makubaliano
17.1 Makubaliano haya ya mkataba, yameridhiwa na pande zote mbili na matakwa yake,
kifungu chochote katika mkataba huu kitabadilishwa kwa taarifa ya maandishi na hayatodhulu
vifungu vingine vya mkataba huu.
18. Kuzuia
18.1 Pande zote za mkataba huu zitambue kifungu chochote kilichokosewa au chenye
mkanganyiko hakiwezi kuufanya mkataba huu kuwa batili au kuzuia usifanye kazi, kitatolewa
au kufanyiwa mabadiliko, vifungu au ibara nyingine zitaendelea kufanyakazi bila kudhulu
taratibu zozote za ajira na mkataba husika.
19. Ufanyaji kazi wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (sheria kuu) Sura ya 366, 2004
19.1 Makubaliano haya yatatafsiriwa na kufanyakazi kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na
Mahusiano kazini Na. 6 ya 2004 na sheria nyingine zitakazoongezwa baadae.
20. Mkataba huu unashuhudia haya yafuatayo;
20.1 Mwajiriwa atatakiwa;
i. Mwajiriwa atawajibika kufanya kila jambo ambalo ujumla wake atahakikisha mafanikio ya
kampuni.
ii. Mwajiriwa atatakiwa kuonekana nadhifu mda wote awapo kazini.
iii. Mwajiriwa atatakiwa kuripoti kazini masaa … … … … … … …kabla ya kipindi, tayari kwa
matayarisho ya shughuli zake za siku na ataingia studio dakika … … … … …kabla kuanza kwa
kipindi, (Muda wa kuanza na kumaliza kazi unaweza kubadilika kufuatia utaratibu wa mkuu wa
idara).
iv. Mwajiriwa atatakiwa kuwajibika katika kuandaa vyema kipindi chake au vifaa muhimu (mgeni)
kwa unadhifu mkubwa.
v. Mwajiriwa atahakikisha anao ufahamu wa kutosha wa kile anachotakiwa kuzungumza au
kupromoti.
vi. Mwajiriwa atafanya matangazo kwa umakini na umahiri mkubwa ili kuhakikisha kuwa wateja
wetu wananufaika na juhudi zake.
vii. Mwajiriwa atatawajibika kwa Mkuu wa kazi (Mkuu wa Idara/Mkuu wa kipindi) kwa utendaji
wake wa kila siku.
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 8
viii. Mwajiriwa atatakiwa kuhudhuria mikutano ya tathmini pamoja na Watendaji wengine wa timu
yake kila siku/wiki.
ix. Ili kuhakikisha mafanikio Mwajiriwa atatakiwa kutekeleza maelekezo ya kiongozi wake wa Idara
au kipindi.
x. Ambapo matangazo yanapaswa kuanza kwa muda uliopangwa na ucheleweshaji wa jambo lolote
linalohusiana na utangazaji hautavumiliwa au kukubaliwa.
xi. Masharti ya nyongeza katika mkataba huu ni;
… … … … …. … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
… … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … …
… … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 9
KWA USHUHUDA HUU, pande zote mbili zinaweka sahihi zao katika Mkataba huu siku na
tarehe kama ilivyo hapa chini.
Imesainiwa Iringa na;
… … … … … … … … … … … … … … … … …
Jina la Mwajiriwa
… … … … … … … … … … … … … … … … …
Tarehe
… … … … … … … … … … … … … … … … …
Sahihi ya Mwajiriwa
… … … … … … … … … … … … … … … … …
MATUMIZI YA KAMPUNI
Jina la Mwajiri/Mwakilishi
… … … … … … … … … … … … … … … … …
Tarehe
… … … … … … … … … … … … … … … … …
Sahihi ya Mwajiri/mwakilishi
… … … … … … … … … … … … … … … … …
WADHIFA
Mbele yangu;
JINA: ……………………………….
SAHIHI: ……………………………….
ANWANI: ……………………………….
WADHIFA: ……………………………….
Imeandaliwa na;
Luther Akyoo
Meneja Rasilimali Watu
Radio Ebony FM.

Contenu connexe

Tendances

PPT on Provident fund New Amendments 2020 : THE EMPLOYEES' PROVIDENT FUNDS AN...
PPT on Provident fund New Amendments 2020 : THE EMPLOYEES' PROVIDENT FUNDS AN...PPT on Provident fund New Amendments 2020 : THE EMPLOYEES' PROVIDENT FUNDS AN...
PPT on Provident fund New Amendments 2020 : THE EMPLOYEES' PROVIDENT FUNDS AN...PradiptaKumarRout
 
Gratuity ppt final
Gratuity ppt finalGratuity ppt final
Gratuity ppt finalTax 2win
 
Employment agreement
Employment agreementEmployment agreement
Employment agreementpsy_syc
 
TDS rate for the financial year 2022-2023
TDS rate for the financial year 2022-2023TDS rate for the financial year 2022-2023
TDS rate for the financial year 2022-2023Masum Gazi
 
Contract of employment
Contract of employmentContract of employment
Contract of employmentCapStone5
 
Statutory Compliance for HR
Statutory Compliance for HRStatutory Compliance for HR
Statutory Compliance for HRshreyasawanto7
 
PF revised wage ceiling limit and its impact
PF revised wage ceiling limit and its impactPF revised wage ceiling limit and its impact
PF revised wage ceiling limit and its impactGreytip Software
 
The payment of gratuity act,1972
The payment of gratuity act,1972The payment of gratuity act,1972
The payment of gratuity act,1972Agile Informatics
 
THE PAYMENT OF BONUS ACT,1965
THE PAYMENT OF BONUS ACT,1965THE PAYMENT OF BONUS ACT,1965
THE PAYMENT OF BONUS ACT,1965Gurjant Rai
 
Conditions of employment & benefits by Jayadeva de Silva
Conditions of employment & benefits by Jayadeva de SilvaConditions of employment & benefits by Jayadeva de Silva
Conditions of employment & benefits by Jayadeva de SilvaJayadeva de Silva
 
Contracting and subcontracting
Contracting and subcontractingContracting and subcontracting
Contracting and subcontractingRoi Xcel
 
Esic benifits ppt
Esic benifits pptEsic benifits ppt
Esic benifits pptvaseem18
 
Employee state insurance act 1948 Benefits
Employee state insurance act 1948 BenefitsEmployee state insurance act 1948 Benefits
Employee state insurance act 1948 BenefitsYogesh Pawar
 
Apprentice act 1961
Apprentice act 1961Apprentice act 1961
Apprentice act 1961vanitha a
 

Tendances (20)

Esi & pf
Esi & pfEsi & pf
Esi & pf
 
Employee Provident Fund Act
Employee Provident Fund ActEmployee Provident Fund Act
Employee Provident Fund Act
 
LEAVE POLICY
LEAVE POLICYLEAVE POLICY
LEAVE POLICY
 
PPT on Provident fund New Amendments 2020 : THE EMPLOYEES' PROVIDENT FUNDS AN...
PPT on Provident fund New Amendments 2020 : THE EMPLOYEES' PROVIDENT FUNDS AN...PPT on Provident fund New Amendments 2020 : THE EMPLOYEES' PROVIDENT FUNDS AN...
PPT on Provident fund New Amendments 2020 : THE EMPLOYEES' PROVIDENT FUNDS AN...
 
E.S.I. Act 1948
E.S.I. Act 1948E.S.I. Act 1948
E.S.I. Act 1948
 
Gratuity ppt final
Gratuity ppt finalGratuity ppt final
Gratuity ppt final
 
INCOME FROM SALARY
INCOME FROM SALARYINCOME FROM SALARY
INCOME FROM SALARY
 
Labour laws in India
Labour laws in IndiaLabour laws in India
Labour laws in India
 
Employment agreement
Employment agreementEmployment agreement
Employment agreement
 
TDS rate for the financial year 2022-2023
TDS rate for the financial year 2022-2023TDS rate for the financial year 2022-2023
TDS rate for the financial year 2022-2023
 
Contract of employment
Contract of employmentContract of employment
Contract of employment
 
Statutory Compliance for HR
Statutory Compliance for HRStatutory Compliance for HR
Statutory Compliance for HR
 
PF revised wage ceiling limit and its impact
PF revised wage ceiling limit and its impactPF revised wage ceiling limit and its impact
PF revised wage ceiling limit and its impact
 
The payment of gratuity act,1972
The payment of gratuity act,1972The payment of gratuity act,1972
The payment of gratuity act,1972
 
THE PAYMENT OF BONUS ACT,1965
THE PAYMENT OF BONUS ACT,1965THE PAYMENT OF BONUS ACT,1965
THE PAYMENT OF BONUS ACT,1965
 
Conditions of employment & benefits by Jayadeva de Silva
Conditions of employment & benefits by Jayadeva de SilvaConditions of employment & benefits by Jayadeva de Silva
Conditions of employment & benefits by Jayadeva de Silva
 
Contracting and subcontracting
Contracting and subcontractingContracting and subcontracting
Contracting and subcontracting
 
Esic benifits ppt
Esic benifits pptEsic benifits ppt
Esic benifits ppt
 
Employee state insurance act 1948 Benefits
Employee state insurance act 1948 BenefitsEmployee state insurance act 1948 Benefits
Employee state insurance act 1948 Benefits
 
Apprentice act 1961
Apprentice act 1961Apprentice act 1961
Apprentice act 1961
 

En vedette

En vedette (8)

Employment agreement
Employment agreementEmployment agreement
Employment agreement
 
CRC - Kiswahili version
CRC - Kiswahili versionCRC - Kiswahili version
CRC - Kiswahili version
 
Survey questionaire instrument kiswahili
Survey questionaire instrument kiswahiliSurvey questionaire instrument kiswahili
Survey questionaire instrument kiswahili
 
A Guide To Customer Service Training
A Guide To Customer Service TrainingA Guide To Customer Service Training
A Guide To Customer Service Training
 
7 Pillars Of Customer Service
7 Pillars Of Customer Service7 Pillars Of Customer Service
7 Pillars Of Customer Service
 
Marketing Management
Marketing ManagementMarketing Management
Marketing Management
 
Customer service training[1]
Customer service training[1]Customer service training[1]
Customer service training[1]
 
CUSTOMER SERVICE POWERPOINT
CUSTOMER SERVICE POWERPOINTCUSTOMER SERVICE POWERPOINT
CUSTOMER SERVICE POWERPOINT
 

Mkataba wa ajira

  • 1. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 1 MKATABA WA AJIRA MKATABA HUU unafanyika leo tarehe ………… mwezi …………………., 2014. BAINA YA … … … … … … … … … … …, wa S.L.P ………………… (ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama “Mwajiri”) wa upande mmoja wapo wa Mkataba NA … … … … … … … … … … … , wa S.L.P ………………….. (ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama “Mwajiriwa”) Namba ya Ajira (I.D). Umri: Jinsia: NSSF Na: Dini: Tarehe ya kuzaliwa: Sehemu ulipozaliwa: Jina la Mke: Tarehe aliyozaliwa Mke: Jina la Mtoto/Watoto: Tarehe ya kuzaliwa Mtoto/Watoto: 1. 2. 3. Dealing with:-Radio Broadcasting, P.A. system and General Entertainment P.O. Box 70270 DAR ES SALAAM TEL: +255 26 2701114 Fax +255 26 2701115, Mob: +255 784 877788, Email: radioebony@ebonyfm.com
  • 2. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 2 MTU WA KARIBU; Jina kamili: … … … … … … … … … … … … … … Umri … … … … Anuani/Mawasiliano: S.L.P … … … … … Simu … … … … … … … … Anapoishi sasa: … … … … … … … Makazi ya kudumu … … … … … . AMBAPO 1. Mwanzo (a) Mwajiri ni Kampuni iliyopo Iringa inayoshughulika na Matangazo ya Radio. (b) Mwajiriwa anafanya Shughuli Iringa na sehemu yeyote atakayopangiwa na mwajiri wake ndani ya utaratibu wa kazi. 2. Wakati wa kuanza kazi 2.1 Mwajiri anakusudia kumwajiri kwa muda wa mwaka/miaka … … … … … mwajiriwa, endapo mkataba huu utaisha utaongezwa/utaendelea kwa matakwa ya kampuni. 2.2 Mahali ulipoajiriwa … … … … … … … … … … … 2.3 Kituo cha kazi … … … … … … … … … … … … .. 2.4 Kazi zako 2.4.1 Nafasi kazini … … … … … … … … … … … 2.4.2 Ripoti kwa … … … … … … … … … … … … 2.4.3 Kazi utapangiwa na … … … … … … … … … Mwajiriwa anakubali matakwa ya mwajiri na anakubali kwa hiari yake mwenyewe kuajiriwa kwa muda wa mwaka/miaka … … … … … kama … … … … … … … … … … 3. Majaribio 3.1 Mkataba huu wa ajira unatambua mda wa majaribio usiopungua miezi mitatu (3) toka siku mwajiriwa alipopata ajira husika. Lengo la mda wa majaribio ni kumpima mwajiriwa kama anakidhi vigezo na viwango vya nafasi/kazi husika. Kama mkataba huu utavunjwa ndani ya mda wa majaribio mwajiriwa atapewa notisi ya maandishi ya siku saba ya kuvunjwa kwa mkataba huu.
  • 3. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 3 3.2 Mda wa majaribio unaweza kuongezwa au kupunguzwa na mwajiri pale atakapoona ni vyema kufanya ivyo, Mwajiri anaweza kuongeza mda wa majaribio hadi miezi kumi na miwili (12). 3.3 Kikomo cha mda wa majaribio, Mwajiri atatakiwa kumfahamisha mwajiriwa kwa maandishi kuchaguliwa kwake katika ajira, kama tu akupata taarifa katika mkataba wake, mwezi mmoja baada ya kuisha mda wa majaribio. 4. Ujira 4.1 Kima cha malipo ya jumla kabla ya makato ya kisheria ni Tshs ….…………. kwa mwezi kulingana na masaa 45 ya ufanyajikazi kwa wiki au kwa taswira ya kampuni husika. 4.2 Mwajiriwa atakatwa makato yanayotambulika kisheria; - Mifuko ya Jamii (NSSF) au Mfuko wa chaguo lako. - Pay As Your Earn (P.A.Y.E). - Sahihi ... ... ... ... ... ... ... ... ... 4.3 Mwajiriwa atatakiwa kuwa na akaunti ya benki, kwajili ya malipo ya Ujira wake; 4.4 Akaunti ya Benki … … … … … … … … … … … … … … … … … ... 5. Saa za kazi 5.1 Mda wa kazi kwa ujumla ni masaa 45 kwa wiki, ila kutokana na taswira na muundo wa kampuni, haswa kituo cha matangazo mwajiriwa atatakiwa kufata Taratibu na Kanuni zilizowekwa na kampuni husika bila kudhuru kifungu chochote cha mkataba huu. 5.2 Mwajiriwa atatakiwa kutambua kituo hichi cha Matangazo kinafanya kazi masaa ishirini na nne (24) kwa siku saba(7) za wiki, ivyo sikukuu za umma zikiangukia katika siku za kazi hakutokuwa na malipo ya ziada au mapumziko kwa watangazaji wa vipindi husika katika siku hiyo. 5.3 Kila mwajiriwa atapata siku moja (1) ya mapumziko ndani ya wiki (siku saba) kulingana na atakavyopangiwa na mkuu wake wa Idara. 6. Likizo 6.1 Mwajiriwa ana haki ya kupata likizo ya siku zisizopungua 28 katika mzunguko wa likizo ya kila mwaka, siku hizo zitajumuisha sikukuu za umma zitakazoangukia ndani ya likizo husika. Likizo itatolewa ndani ya miezi kumi na miwili (12) toka kuanza kwa ajira yako. Au baada ya kuisha kwa mzunguko wa awali katika ajira.
  • 4. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 4 6.2 Likizo itatolewa na mwajiri pale atakapoona ni wakati mwafaka kufanya ivyo, na kumjulisha mwajiriwa. 6.3 Idadi ya siku za likizo zinaweza kugawanywa na mwajiri katika mda tofauti ndani ya mzunguko wa likizo bila kudhuru idadi ya siku za likizo za mfanyakazi. 6.4 Mwajiri hatoomba au kuombwa na mwajiriwa kufanya kazi ndani ya mda wa likizo. 7. Likizo ya Ugonjwa 7.1 Kulingana na kifungu cha 32 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (Sheria kuu) Sura ya 366, mwajiriwa atapata likizo ya Ugonjwa kwa siku 126 katika mzunguko wa likizo na malipo yake halali, ikiwa tu, ugonjwa huo umethibitishwa na vyeti cha tatibu aliesajili au tabibu anayekubalika na mwajiri. 7.2 Likizo ya Ugonjwa iliyotajwa katika kifungu kidogo cha (1) italazimika kukokotolewa kama ifuatavyo; 7.2.1 Siku 63 za kwanza zitatakiwa kulipwa mshahara mzima, 7.2.2 Siku 63 zinazofuata zitatakiwa kulipwa nusu mshahara 7.2.3 Mwajiri ana haki ya kuvunja mkataba wa ajira baada ya siku 126 za likizo ya Ugonjwa kupita. 7.2.4 Mwajiriwa anatakiwa kutoa taarifa za ugonjwa haraka iwezekanavyo kwa mwajiri. 8. Likizo ya Uzazi 8.1 Mfanyakazi atalazimika kutoa notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua na notisi hiyo italazimika kuambatana na cheti cha kitabibu. 8.2 Vile vile Mwajiriwa atatakiwa kufata taratibu zote za Likizo ya Uzazi kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 33 – kifungu kidogo (2) hadi (11), Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (Sheria kuu) Sura ya 366. 9. Likizo ya uzazi ya baba na aina nyingine za likizo 9.1 Wakati wa Mzunguko wa likizo, Mfanyakazi atakuwa na haki ya; 9.1.1 Angalau siku 3 za likizo ya uzazi ya baba kama- (a) Likizo itachukuliwa ndani ya siku saba za kuzaliwa mtoto na; (b) Mfanyakazi ni baba wa mtoto; 9.1.2 Angalau siku 4 za likizo kwa sababu zifuatazo; (a) Ugonjwa au kifo cha mtoto wa mfanyakazi;
  • 5. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 5 (b) Kifo cha mke wa mfanyakazi, wazazi, bibi na babu, mjukuu au kitukuu. Mwajiri anaweza kuhitaji uthibitisho wa kawaida wa tukio lolote lililotajwa hapo juu. 10. Kusitishwa kwa Ajira 10.1 Mkataba huu unaweza kusitishwa na pande zote mbili kwa notisi ya siku zisizopungua 28. 10.2 Notisi inatakiwa kutolewa kwa maandishi, ikieleza sababu na tarehe ya kusitishwa ajira husika. 10.3 Endapo mwajiri atasitisha ajira, anatakiwa kumpa mfanyakazi Cheti. 10.4 Hata ivyo, Mwajiri ana haki ya kutotoa Cheti hadi pale Mfanyakazi atakaporudisha mali au thamani yeyote ya kampuni. 10.5 Mwajiri atasitisha ajira husika endapo mfanyakazi atashindwa kufata matakwa ya mkataba huu, taratibu, kanuni na miongozo ya kampuni. 11. Malipo ya Kiinua Mgongo 11.1 Mfanyakazi ana haki ya kupata kiinua mgongo cha mshahara angalau wa siku 7 kwa kila mwaka ulioisha wa utumishi wa moja kwa moja na mwajiri mpaka kwa kiwango cha juu cha miaka kumi (10), 11.2 Mwajiri atatakiwa kumlipa kiinua mgongo wakati wa kusitisha ajira ikiwa; (i) Mfanyakazi amemaliza miezi 12 ya utumishi wa moja kwa moja na mwajiri 11.3 Mfanyakazi hatopata kiinua mgongo kama; 11.3.1 Kama ajira yake ilisitishwa kwa utovu wa nidhamu 11.3.2 Kama amegoma kufanya kazi alizopangiwa kwa taratibu za ofisi 12. Biashara Binafsi 12.1 Wafanyakazi wote ni waajiriwa wa kudumu, ivyo mfanyakazi yeyote hatoruhusiwa kufanya biashara wakati wa kazi au mda wa kazi. 12.2 Kwenye jengo la kampuni; 12.3 Au kutumia mali, au chombo chochote cha kampuni kuwezesha biashara yake; 12.4 Au kuwatumia waajiriwa wengine wa kampuni hii kufanikisha biashara yake ndani ya mda wa kazi. Hairuhusiwi. 13. Usiri 13.1 Uendeshaji wa biashara, utendaji na mipango ya kampuni ni vitu vinavyohitaji usiri wa hali ya juu, ivyo nyaraka, taarifa, kumbukumbu za kimaandishi, muktasari wa vikao vya ndani,
  • 6. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 6 ulipaji wa mishahara, uendeshaji wa kampuni utalindwa kwa usiri mkubwa, na chochote hakitakiwi kumhusisha mtu hasie wa kampuni bila idhini ya utawala. Ukibainika kuvunja usiri huu unaweza kupoteza ajira yako. 14. Utoro 14.1 Mfanyakazi hatotakiwa kukosa kazini katika siku za kazi bila ruhusa ya mwajiri au uongozi husika. 14.2 Mfanyakazi akitoweka/utoro kazini bila taarifa katika siku tano (5) za kazi, mwajiri atahesabu upotevu/usitishwaji wa ajira ya mfanyakazi huyo toka siku ya kwanza ya utoro huo 14.3 Mimi, … … … … … … … … … … … … … … natambua utoro kazini utapelekea kupoteza ajira yangu, natambua kutoonekana kazini kwa siku zisizopungua tano(5) ni uvunjifu wa mkataba na taratibu za ofisi, ivyo kampuni ihesabu utoro wangu ni sehemu ya kujiuzulu. 14.4 Utoro wa vikao vya alhamisi mara tatu (3) ndani ya mwezi moja (1) vilivyowekwa kwa utaratibu wa kampuni, unaweza kukufikisha katika kamati ya nidhamu au kukusabishia rekodi hafifu ndani ya mwaka wa ajira, ivyo kuchangia kupoteza ajira yako. 15. Utovu wa Nidhamu 15.1 Wafanyakazi wote wanatakiwa kuheshimu na kufata sheria, taratibu na kanuni za kampuni. Mwajiriwa yeyote atakae shindwa kuheshimu taratibu hizo atachukuliwa hatua kali za inidhamu, au kupoteza ajira yake. 16. Masharti ya Ushindani 16.1 Kulingana na taratibu na kanuni na sheria ya Ajira na Mahusiano kazini, mfanyakazi yeyote atapaswa kufata taratibu za kusitisha ajira, endapo mfanyakazi halali wa Redio Ebony FM mwenye mkataba atatoroka na kwenda kufanya kazi sehemu nyingine bila kufata utaratibu hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 16.2 Mfanyakazi yeyote hatoruhusiwa kufanya kazi yenye mfanano na kampuni hii akiwa ndani ya ajira husika. 16.3 Ni kosa kwa mfanyakazi wa Ebony FM kufanyakazi na kituo kingine cha matangazo akijua yeye ni mwajiriwa wa halali wa kampuni tajwa. 16.4 Kufanya au kuuza vipindi, vionjo au muundo wa vipindi vya kampuni ni kosa kisheria, hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakaebainika.
  • 7. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 7 17. Makubaliano 17.1 Makubaliano haya ya mkataba, yameridhiwa na pande zote mbili na matakwa yake, kifungu chochote katika mkataba huu kitabadilishwa kwa taarifa ya maandishi na hayatodhulu vifungu vingine vya mkataba huu. 18. Kuzuia 18.1 Pande zote za mkataba huu zitambue kifungu chochote kilichokosewa au chenye mkanganyiko hakiwezi kuufanya mkataba huu kuwa batili au kuzuia usifanye kazi, kitatolewa au kufanyiwa mabadiliko, vifungu au ibara nyingine zitaendelea kufanyakazi bila kudhulu taratibu zozote za ajira na mkataba husika. 19. Ufanyaji kazi wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini (sheria kuu) Sura ya 366, 2004 19.1 Makubaliano haya yatatafsiriwa na kufanyakazi kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6 ya 2004 na sheria nyingine zitakazoongezwa baadae. 20. Mkataba huu unashuhudia haya yafuatayo; 20.1 Mwajiriwa atatakiwa; i. Mwajiriwa atawajibika kufanya kila jambo ambalo ujumla wake atahakikisha mafanikio ya kampuni. ii. Mwajiriwa atatakiwa kuonekana nadhifu mda wote awapo kazini. iii. Mwajiriwa atatakiwa kuripoti kazini masaa … … … … … … …kabla ya kipindi, tayari kwa matayarisho ya shughuli zake za siku na ataingia studio dakika … … … … …kabla kuanza kwa kipindi, (Muda wa kuanza na kumaliza kazi unaweza kubadilika kufuatia utaratibu wa mkuu wa idara). iv. Mwajiriwa atatakiwa kuwajibika katika kuandaa vyema kipindi chake au vifaa muhimu (mgeni) kwa unadhifu mkubwa. v. Mwajiriwa atahakikisha anao ufahamu wa kutosha wa kile anachotakiwa kuzungumza au kupromoti. vi. Mwajiriwa atafanya matangazo kwa umakini na umahiri mkubwa ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wananufaika na juhudi zake. vii. Mwajiriwa atatawajibika kwa Mkuu wa kazi (Mkuu wa Idara/Mkuu wa kipindi) kwa utendaji wake wa kila siku.
  • 8. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 8 viii. Mwajiriwa atatakiwa kuhudhuria mikutano ya tathmini pamoja na Watendaji wengine wa timu yake kila siku/wiki. ix. Ili kuhakikisha mafanikio Mwajiriwa atatakiwa kutekeleza maelekezo ya kiongozi wake wa Idara au kipindi. x. Ambapo matangazo yanapaswa kuanza kwa muda uliopangwa na ucheleweshaji wa jambo lolote linalohusiana na utangazaji hautavumiliwa au kukubaliwa. xi. Masharti ya nyongeza katika mkataba huu ni; … … … … …. … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … … .
  • 9. Mkataba, Radio Ebony FM, 2014 Page 9 KWA USHUHUDA HUU, pande zote mbili zinaweka sahihi zao katika Mkataba huu siku na tarehe kama ilivyo hapa chini. Imesainiwa Iringa na; … … … … … … … … … … … … … … … … … Jina la Mwajiriwa … … … … … … … … … … … … … … … … … Tarehe … … … … … … … … … … … … … … … … … Sahihi ya Mwajiriwa … … … … … … … … … … … … … … … … … MATUMIZI YA KAMPUNI Jina la Mwajiri/Mwakilishi … … … … … … … … … … … … … … … … … Tarehe … … … … … … … … … … … … … … … … … Sahihi ya Mwajiri/mwakilishi … … … … … … … … … … … … … … … … … WADHIFA Mbele yangu; JINA: ………………………………. SAHIHI: ………………………………. ANWANI: ………………………………. WADHIFA: ………………………………. Imeandaliwa na; Luther Akyoo Meneja Rasilimali Watu Radio Ebony FM.